June 17, 2019


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe,  amewaomba Watanzania kuichangia Timu ya Taifa (Taifa Stars) ambayo ipo Misri kwa ajili ya michuano ya #AFCON2019

Mwakyembe amesema hayo leo Jumatatu, Juni 17, 2019 wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maandalizi ya Stars ykwa ajili ya fainali za  AFCON.

“Siku ya Alhamisi asubuhi tutakuwa na zoezi kubwa ambalo litaluwa LIVE kwenye mitandao na television mbalimbali na kwenye radio ambapo tutafanya uchangiaji wa Taifa Stars. Nawahakikishia kila shilingi itakayopatikana itakwenda kwa vijana wetu, wasishindwe kwa kuvunjika moyo,” amesema.

Amesisitiza kwamba fedha zitakazochangwa si kwa ajili ya kuipeleka timu Misri na kuirudisha, “hatuhitaji kuwaweka kwenye hoteli nzuri (hayo yote yameshafanyika) tunahitaji kufanya kitu ili timu yetu ifanye vizuri.

“Leo hii Tanzania inajivunia kwamba ukitaja ma-striker wakubwa duniani huwezi ukamkosa Samatta, Mungu atupe nini? Ndiyo kipindi chetu, dunia sasa hivi inatambua Tanzania ipo mpaka hapa tulipofikia,” amesema Dkt. Mwakyembe.

2 COMMENTS:

  1. Timu ya taifa sio ya kuomba kuomba sh 100 .nafikiri gorv itambue ilo.

    ReplyDelete
  2. FIFA & CAF ni mashindano makubwa pesa za ushiriki ziko wapi na ngapi kwa washiriki ikiwemo taifa stars mbona hakuna uwazi katika hilo?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic