June 19, 2019


Yanga kweli ni kubwa kuliko, Juni 15, 2019 ilidhihirisha wakati walipofanya hafla yao ya harambee ya kuchangishana fedha, pia ilitambulisha nyota wake wapya akiwamo mchana nyavu waliyempora kutoka kwa watani wao Simba Juma Balinya.


MAJALIWA ATAKA YANGA IMARA

Mgeni rasmi Kassim Majaliwa katika salamu zake aliipongeza Yanga kwa kuwa licha ya kucheza ligi msimu uliomalizika lakini walipambana vikali na kushika nafasi ya pili na kwamba hawakubebwa.

“Yanga ilikuwa na hali mbaya, lakini ilipambana yenyewe na kushika nafasi ya pili niwapongeze sana na niseme Yanga haikubebwa ilipambana,” alisema Majaliwa. 

Aidha Majaliwa alimpongeza Kocha Mwinyi Zahera akisema kocha huyo ni kocha mzuri ambaye alioisaidia klabu hiyo.

“Mimi kitaaluma ni kocha pia ni mkufunzi niseme Zahera ni kocha mzuri aliyeisaidia sana Yanga, mwisho niseme hakuna Ligi bora bila Yanga imara na hakuna simba imara bila Yanga imara.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic