UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa umekamilisha mchakato wa usajili wa wachezaji wake kwa asilimia 90 kutokana na maagizo ya kocha Mkuu, Mwinyi Zahera.
Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla amesema kuwa usajili wote walioufanya umetegema ripoti ya kocha hivyo wana imani wataleta ushindani kwenye michuano ya kimataifa.
"Kazi ya usajili tumeifanya kwa kuzingatia matakwa ya kocha, imani yetu tutafanya kweli kwenye michuano ya ndani na ya kimataifa," amesema Msolla.
Mashine mpya ambazo zimesajiliwa ni pamoja na Patrick Sibomana, Lamine Moro, Issa Bigirimana, Maybin Kalego, Mustapha Suleiman, Juma Balinya, Sadney Urikhob na Abdulaziz Makame.
Lamine Moro, Juma Balinya na Sadney wote hao walikataliwa na Simba!
ReplyDeleteKwani simba inamzani yakupimia wachezaji
DeleteKwani simba inamzani yakupimia wachezaji
DeleteWaache watapetape mwisho Wa Rambo ndio huo.
ReplyDelete