AJIBU AKUTANA NA PACHA ZAKE SIMBA, BONGE LA SELFIE LAPIGWA
Wachezaji Mohammed Hussein, Said Ndemla na Ibrahim Ajibu wamekutana katika picha ya pamoja leo.
Utatu huo umekutana tena baada ya misimu miwili iliyopita Ajibu kuwa Yanga lakini sasa amerejea tena kunako Simba SC.
Ajibu amerejea baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili na sasa atahudumu Simba mpaka mwaka 2021.
Watatu hao wamepiga SELFIE hiyo ya pamoja kabla ya semina maalum juu ya wachezaji wote wa Simba kuanza leo ambapo ilikuwa inahusiana na masuala mbalimbali juu yao kutoka kwa uongozi.
0 COMMENTS:
Post a Comment