July 18, 2019


IDD Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa kesho watapambana kuwakalisha wapinzani wao Manyema FC kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la Kagame.

Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa wametambua ubora na uimara wa wapinzani wao hivyo watawamaliza mapema.

"Wapinzani wetu wapo imara, tumewaona kwenye mchezo wao dhidi ya APR, sasa tumejipanga kupata matokeo chanya hasa ukizingatia ni hatua ya nusu fainali hivyo kikubwa ni sapoti na kujituma," amesema Cheche.

Azam FC ni mabingwa watetezi wa kombe la Kagame wametinga hatua ya nusu fainali baada ya kuwanyoosha TP Mazembe mabao 2-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic