MSIMU mpya
wa 2019-20 unakaribia kuanza kwani kwa sasa hakuna siku nyingi ambazo zimebaki
kabla ya Ligi Kuu Bara kuanza.
Tayari Bodi
ya Ligi Tanzania imetangaza ratiba ambayo inaonyesha kwamba Agosti 23 ligi
itaanza kurindima kwenye viwanja mbalimbali hapa nchini.
Ni kitu
kizuri kwa ligi kuanza ila maumivu makubwa bado yapo nyuma ya ligi kutokana na
namna mambo yanavyokwenda kimyakimya.
Ninaona
kwamba msimu ujao bado haujawa kwenye mpango bora ambao upo na unataka kuwa
kama wengi ambavyo wanafikiria.
Ikumbukwe
kuwa hata msimu uliopita baada ya ratiba kujulikana hakuna ambaye alionekana
kujali kila kitu kilikwenda kimyakimya kuhusu maandalizi.
Siku ya ligi
kuanza kalenda zikaanza hasa kwenye suala la mdhamini mkuu na Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) likaweka bayana kwamba mzunguko wa pili mambo yatakuwa
safi.
Ahadi yao
ilikuwa kwamba wanazungumza na mdhamini mkuu hivyo watamtangaza baada ya
kufika makubaliano picha iliendelea mpaka mzunguko wa pili mambo yakawa ni
kimya.
Mpaka sasa
bado habari ni zilezile kama msimu uliopita ndivyo ambavyo naona tunakwenda
hali imeshaanza kuwa mbaya.
Kwa mdhamini
mkuu hakuna anayegusia na wala hakuna dalili zozote za wazi zinazonesha kwamba
msimu ujao kutakuwa na utofauti.
Mdhamini
hajatangazwa mpaka muda huu ambapo timu tayari zimeanza maandalizi ya awali
huku nyingine zikiwa zinakwenda kuweka kambi.
Kumbukumbu
zangu zinaniambia kwamba ahadi ilikuwa msimu ujao tutakuwa na mdhaminini mkuu
ambaye atasaidia kupunguza changamoto za ligi.
Nina mashaka
hata msimu ujao mambo bado yatakuwa magumu kwa timu nyingi ambazo zinashiriki
ligi kama hatua hazitachukuliwa.
Kuna timu
nyingi za ligi mpaka sasa hazijakamilisha usajili hata mchezaji mmoja zaidi
zinabomolewa tu.
Wachezaji
wao wanachukuliwa na timu zenye hela huku wao wakibaki wakiwatazama wachezaji
wao wanaowapenda.
Pia tatizo
kubwa lipo kwa timu nyingi hazijakamilisha malipo ya wachezaji kwa muda wa
miezi mitatu mpaka sita.
Hii yote
inatokana na ukata uliopo hasa kwa timu kushindwa kuwa na fedha za kujikimu na
kujiendesha hasa msimu uliopita na huu wa sasa.
Hebu pata
picha timu hizi Lipuli, Ndanda, Biashara United, Alliance FC na Mwadui bado
hawajafanya usajili makini.
Achana na
usajili huu ambao wanaufanya kwa sasa bado sio malengo yao kwani wana madeni
makubwa kwa msimu uliopita
Hawa wote
wanadaiwa kuanzia kwa walimu na wachezaji wanawadai mishahara na uwezo walionao
ni wa kuunga tu sio kama wanapenda kufanya hivyo hawana namna.
Walimu
wanadai na bado wanahitajika kufundisha hapo ndipo unapopata mtindo wa timu zetu
zilivyo na mipango yao inavyoanza kuyumba mwanzo kabisa kabla ya ligi yenyewe
kuanza.
Wachezaji
wanadai ni haki yao na hawana mpango wa kucheza kwa morali kama ilivyokuwa
awali ndio maana wengi waliopata dili la kusepa walitimka bila kuangalia ni
timu daraja gani anakwenda kutumikia.
Mchezaji ni
mfanya biashara ila muda mwingine thamani yake inabebwa na timu ambayo
anaitumikia hivyo muda wa kujipanga kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ni sasa.
Hakuna atakayekubali
kufanya kazi muda mrefu bila kuwa na fedha ambazo zitamsaidia kuendesha maisha
yake ya kila siku.
TFF wakae
chini ili kuona namna gani msimu ujao utakavyokuwa, waache maneno, watimiza
ahadi ambayo walitoa wao wenyewe kwa timu zote kupitia kwa Rais.
Bado mambo
ni magumu nao wapo kimya nakumbuka msimu uliopita wengi walipewa taarifa ayari ligi
imeanza kwamba hakuna mdhamini timu zitajiendesha zenyewe na
matokeo yake ligi ikiwa inakwenda kwa kusuasua.
Wanapaswa
wafanye jambo la ziada kumpata mdhamini ili kuboresha ligi ambayo awali mechi
za mwanzo zilianza kuwa na ushindani ila katikati matatizo yalianza kujitokeza.
Mpira ni
pesa na uwekezaji ni kitu muhimu na hili suala TFF hawawezi kulikwepa kwa kuwa
ni jukumu lao kuhakikisha soka letu linakuwa na sio kudumaa kila siku.
Ubora wa
ligi ya ndani unasaidia kukuza wachezaji wetu wa ndani na kuwafanya wawe bora
muda wote kwenye michuano ya ndani na ile ya kimataifa.
Tunataka
kuona wachezaji wengi wa ndani wanapata dili la kucheza nje ya nchi na haya
hayatokei kwa bahati mbaya ni lazima timu zijipange na TFF nao wawe na mipango
makini.
Rai yangu
kwa TFF hili wasilichukulie kiwepesi hasa kwa wakati huu ambao dunia
inakimbizana na mafanikio ya soka.
Ivi TFF hawana kitengo cha marketing?
ReplyDeleteTutabaki kulaumu sana makocha wa timu ya taifa kitu ambacho siyo sahihi! Udhamini bora wa ligi utachangia sana upatikanaji wa wachezaji bora watakaosaidia kukuza ubora wa timu ya taifa na kutufanya tu move forward zaidi ya tulipo kwa sasa kisoka
ReplyDeleteSponsors wanaangalia benefits watazopata kutokana na udhamini walioufanya! No company will sponsor where they no the people who are there are not determined to ensure the mutual benefits
ReplyDeleteMambo ya TFF wanashangaza sana,timu hazina fedha,hawalipwi halafu wananufaika na faini kibao
ReplyDeleteMbona Yanga hawajapata mdhamini hamuwasemi?
ReplyDeleteBaba kwanza watoto badae! Baba akiwa na foundation nzuri na watoto kuna possibility kubwa na wao kuwa vizuri kifikra
Delete