KOCHA Mkuu
wa Biashara United, Amri Said amesema kuwa timu yake itaweka kambi Tarime kwa
ajili ya maandalizi ya msimu ujao unaotarajiwa kuanza Agosti 23, Julai 20.
Akizungumza na Saleh Jembe, Said amesema kuwa kwa sasa kinachowachelewesha kuanza
kambi ni ukata hivyo mambo yakikaa sawa wataingia kambini.
“Kwa sasa
bado hatujaanza kambi, ilibidi tuanze Julai 15 mambo hayajawa sawa kutokana na
tatizo la uchumi, ila mpaka Julai 20 mambo yatakuwa sawa na lazima tuanze
kujiaanda kwa ajili ya msimu ujao kwani ratiba imebana.
“Timu
itaweka kambi Tarime na tumepanga kucheza mechi nyingi za kirafiki ili kuandaa
kikosi makini, nina mani tutafanya vizuri msimu ujao wadau na mashabiki
waendelee kutupa sapoti,” amesema Said.
0 COMMENTS:
Post a Comment