July 19, 2019


KIUNGO mshambuliaji mpya wa Yanga Mnyarwanda, Issa Bigirimana ‘Walcott’ amesema kuwa katika kuthibitisha ubora wa ufungaji anaanza na AS Vita wanafuatia watani wao Simba.

Staa huyo aliitoa kauli hiyo, akiwa kambini mkoani Morogoro ambako wameingia tangu Jumatatu iliyopita wakijiandaa na msimu mpya wa ligi pamoja na tamasha lao la Wiki ya Mwananchi litakalofanyika Agosti 4, mwaka huu.

Katika tamasha hilo, Yanga wanatarajiwa kucheza mchezo mmoja wa kirafi ki wa kimataifa dhidi ya AS Vita utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Bigirimana alisema kuwa anafahamu uwezo wake, hivyo kwa kuanza atauonyesha kwenye mchezo huo wa kirafi ki dhidi ya AS Vita.

Bigirimana alisema, anafahamu AS Vita wapo baadhi ya wachezaji wanaomfahamu, lakini hilo halimpi shida na badala yake atahakikisha anaonyesha makali yake baada ya kutoka kambini huko Morogoro.

“Ninafahamu Mashabiki wa Yanga wana imani na mimi na kikubwa ninataka kuwathibitishia ubora wangu kwa kuanzia mchezo huu wa kirafi ki dhidi ya AS Vita.

“Baada ya mchezo huo watafuata wapinzani wetu Simba, mchezo ninaousubiria kwa hamu kubwa mara tutakapokutana nao.

“Mimi hizo derby ndiyo ninazozipenda, kikubwa ninataka kuwaonyesha uwezo wangu, katika kila mchezo ninataka kufunga bao ili nitengeneze historia kubwa ndani ya Yanga,” alisema Bigirimana.

9 COMMENTS:

  1. Mziki wa SSC Bado hajaujua kisawasawa kijana.

    ReplyDelete
  2. Bigirimana unaouwezo WA kumchokoza Simba?

    ReplyDelete
  3. Huyu inaelekea hajaelezwa vizuri kuhusu Mnyama.

    ReplyDelete
  4. Apitie wapi kwa kapombe , nyoni , sultani , gadiei au kwa kitasa mbrazil . Labda aje amruchimbia mpira chini ya ardhi

    ReplyDelete
  5. Halafu huyo Bigimana anapishana na kauli ya zuhura ambaye amesema dawa pekee ya kuwadhibiti simba ya mwaka huu atatumia formation ya 9 1 0 kwa maana mabeki 9 , kiungo 1 na hakuna mshambuliaji

    ReplyDelete
  6. Yaani simba maneno mengi mpaka mnaharibu ladha za habari

    ReplyDelete
  7. Simba mnayoiogopa ni IPI? Ile iliyopigwa tano na As vita, iligopigwa tano na All Hahli au ile iliyocheza na yanga ikapiga pasi elfu kumi na kupata goli moja?

    ReplyDelete
  8. Mimi naiogopa Ile iliyoichapa yanga 6/0

    ReplyDelete
  9. Ama Mimi naiogopa Ile iliyofika robo fainali na kuiwezesha Yanga nayo kushiriki mashindano hayo mwaka huu bila ya kutoka jasho

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic