July 19, 2019



DEOGRATIUS Munish 'Dida' inaelezwa kuwa anawindwa na timu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar ili kuziba pengo la Benedict Tinnoco ambaye amejiunga na Kagera Sugar.

Dida kwa sasa ni mchezaji huru ambaye mkataba wake na Simba umekamilika na hajaongezewa mwingine.

Dida amesema kuwa bado yupo kwenye mazungumzo na timu nyingi ambazo zinahitaji huduma yake wakati ukifika atazitaja.

"Kuna timu nyingi ambazo nipo nazo kwenye mazungumzo, muda ukifika nitazitaja, kuna ofa kutoka timu kubwa nje ya Bongo pamoja na nyingine za ndani," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic