July 8, 2019

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kazi kubwa ambayo wataifanya kwenye michuano ya Kagame ni kutetea taji lao.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Azam FC, Ettiene Ndayiragije amesema kuwa ana imani ya kufanya makubwa kwenye michuano hiyo licha ya  tatizo la spidi kwa wachezaji wake kuwa chini.

"Tutatumia nguvu nyingi kupata ushindi kwani kazi yetu ni kutetea ubingwa, bado wachezaji wana spidi ndogo nadhani ni ugeni ila hamna namna kwa kuwa tunatetea kombe ni lazima tupambane kufanya vizuri.

"Mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani michuano hii sio rahisi kama ambavyo wengi wanafikiria," amesema.

Mchezo unaofuata wa Azam FC ni dhidi ya KCCA ya Uganda utachezwa Jumanne. 

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic