July 8, 2019

MAPINDUZI Balama kiungo mpya wa Yanga amesema kuwa kwa sasa anasubiri sauti ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera kumpanga nafasi atakayocheza ndani ya Yanga.

Balama amejiunga na Yanga akitokea Alliance kwa kandarasi ya miaka miwili atakuwa na kazi ya kupambana na viungo wa Yanga ambao ni Papy Tshishimbi, Mohamed Issa 'Banka', Feisal Salum 'Fei Toto' ambao wapo ndani ya kikosi hicho.

"Mwalimu ndiye ana kazi ya kunipa namba na kunipangia sehemu ya kucheza, sina mashaka na uwezo wangu kwani yeye ndiye aliyependekeza nisajiliwe anajua nafasi nitakayocheza," amesema.

Yanga ina mpango wa kuweka kambi mjini Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa mwaka 2019-20.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic