July 17, 2019



NYOTA wanne wa Simba ambao walikwama kukwea pipa na timu kwenda nchini ya Afrika Kusini wanatarajia kusepa muda wowote kuanzia sasa baada ya kukamilisha taratibu zote.

Simba imeweka kambi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mwaka 2019-20 na haikuwa na nyota wake wanne kutokana na kutokuwa na passport.

Wachezaji hao ambao ni Meddie Kagere, Deo Kanda, Francis Kahata na Sharaf Eldin Shoboub Ali Abdalrahman.

Nyota hao kwa sasa wamekamilisha taratibu zote na muda wowote kuanzaia leo watakwea pipa kuelekea Afrika Kusini.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori amesema: "Tumesajili jumla ya wachezaji 26, kikosi cha kwanza, wachezaji wameelekea South Afrika na wengine wakikamilisha passport zao nao watasafiri kuwafata wenzao", amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic