July 17, 2019


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa uzoefu utakibeba kikosi hicho kwenye michuano ya kimataifa kwani rekodi zinaonyesha kwamba kwa Tanzania ni timu ambayo imeshiriki mara nyingi michuano ya kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga msimu huu itapeperusha Bendera ya Taifa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya Tanzania kupata nafasi ya kuongeza timu shiriki na Caf.

Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa hawana shida na michuano ya kimataifa watawatoa kimasomaso mashabiki.

“Hakuna ugeni kwetu kwenye michuano ya kimataifa, rekodi zinaonyesha kwamba tumeshiriki mara nyingi michuano ya Ligi ya Mabingwa hivyo hatuna ugeni na kwa mipango tuliyonayo ni kuleta ushindani.

“Ukitazama kwa sasa kikosi chetu kina sura za kazi na kila mchezaji ana morali kubwa ya kupambana kwa ajili ya timu hivyo suala la kimataifa tunakwenda kifua mbele kwa ajili ya kuipeperusha Bendera ya Taifa,” amesema.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic