July 21, 2019

NYOTA wa timu ya Taifa ya Senegal, Sadio Mane amesema kuwa kilichowaponza washindwe kutwaa kombe la Afcon mwaka 2019 ni kushindwa kutumia nafasi walizozipata.

Senegal imetinga hatua ya fainali ya michuano ya Afrika mara mbili na imeambulia patupu muda wote.

Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2002 na ilifungwa na Cameroon kwa penalti nchini Mali na fainali yake ya pili ikafungwa na Algeria bao la mapema kabisa dakika ya pili nchini Misri.

Mane amesema kuwa kilichowaponza washindwe kupata ushindi ni kushindwa kutumia nafasi walizozipata jambo lililowafelisha.

"Tumeshindwa kutwaa kombe kutokana na kushindwa kutumia nafasi tulizozipata, wenzetu mapema walitumia nafasi waliyoipata hapo ndipo tulipokwama na inaumiza kweli," amesema.

Algeria mara ya mwisho kutwaa taji hilo ilikuwa ni  mwaka 1990 na wamelitwaa tena mwaka 2019 baada ya kupita miaka 29.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic