July 21, 2019


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kilichomchelewesha mlinda mlango wao mpya, Farouk Shikalo kujiunga na timu hiyo ni makubaliano yao na timu yake ya zamani ya Bandari FC.

Shikalo amesajiliwa na Yanga kwa kandarasi ya miaka miwili anatarajiwa kujiunga na timu ya Yanga iliyopo Morogoro muda wowote kuanzia sasa.

Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa taratibu zote zimekamilika hivyo muda wowote atawasili nchini.

"Kikubwa ambacho kimemchelewesha Shikalo kujiunga na timu ni majukumu yake ndani ya timu ya Bandari ambao walimuomba ili wamalize michuano ya Kagame ambayo inafanyika nchini Rwanda.

"Pia yeye alikuwa anachezea timu ya Taifa ya Kenya hivyo alipewa mapumziko maalumu kwa sasa kila kitu kipo sawa muda wowote anatua," amesema.

Bandari kwenye michuano ya Kagame walitolewa hatua ya awali na leo ndio fainali itakayochezwa kati ya Azam FC na KCCA ya Uganda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic