MARCUS Rashford mshambuliaji wa Manchester United leo ameibuka mchezaji bora wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Leeds ambao ni maalumu kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.
United kwa sasa wameweka kambi nchini Australia
na kwenye mchezo wa leo wameibuka na ushindi wa mabao 4-0.
Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa ameshangazwa na uwezo wa Rashford ambaye ametupia pia bao pamoja na kinda Mason Greenwood ambaye ametupia bao lake la kwanza, mabao mengine yalifungwa na Phil Jones pamoja na Martial.
Mchezaji aliyechaguliwa na mashabiki kuwa mchezaji bora kwa mchezo wa leo ni kiungo mshambuliaji Paul Pogba.
0 COMMENTS:
Post a Comment