July 18, 2019


FRANCIS Kahata kiungo mpya wa Simba amesema kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wamechangia kumshawishi ajiunge ndani ya kikosi hicho ni mshambuliaji Meddie Kagere.

Kahata amejifunga kwa kandarasi ya miaka miwili ndani ya Simba akitokea timu ya Gor Mahia ambayo Kagere naye aliwahi kuitumikia.

"Nilikuwa nina ofa nyingi mbali na Simba kutokana na ukubwa wa klabu na ukaribu wangu na Kagere sikuona haja ya kwenda mbali nikakubali kujiunga na Simba.

"Kwa sasa ninafuraha kwa kuwa nimeona timu ipo vizuri na ina mipango mingi mizuri hivyo kwa kushirikiana nao nina amini tutafanya vema," amesema Kahata.

3 COMMENTS:

  1. Hongera zenu kilichobaki kuonesha kazi yenu!

    ReplyDelete
  2. Sasa no muda was kuonesha action uwanjani hayo maneno maneno tuwaachie waandishi

    ReplyDelete
  3. Karibu ndani ya msimbazi chama kubwa africa mashariki na kati

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic