July 18, 2019

OLE Gunnar Solskjaer, meneja wa Manchester United amesema kuwa bado atabaki na nyota wa kikosi hicho Paul Pogba na anaweza kumfanya akawa bora zaidi kwa kuwa hakuna ofa inayomtaka.
United wana kazi ya kumzuia Pogba ambaye anawindwa na Juventus pamoja na Real Madrid huku wakiwa wametaja dau kubwa la kumuza mchezaji huyo la pauni milioni 170.
Pogba na wakala wake Mino Raiola hawajaweka siri mpango wa Pogba kutaka kusepa United msimu ujao.
"Nitampa changamoto mpya na ninaweza, Paul ni mchezaji mzuri na bora hana tatizo lolote na kama atacheza kwa mtindo ule kama wakati ninakuja ndani ya kikosi hiki atakuwa bora zaidi.
"Siwezi kusema chochote kuhusu hatma yake kwa kuwa kumekuwa na mazungumzo mengi juu yake na ninajua kwa dhati kipi ambacho Paul anafikiria na mpaka sasa hatuna ofa yoyote juu yake," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic