July 19, 2019


ODION Ighalo mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Nigeria anatazamiwa kumaliza michuano ya Afcon inayoendelea nchini Misri akiwa mfungaji bora.

Ighalo ni shujaa wa Nigeria kwani aliipa ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo dhidi ya Tunisia ambao ulikuwa wa kumtafuta mshindi wa tatu uliochezwa Jumatano.

Mpaka sasa ametupia mabao matano, akiwaacha kwa mbali washambuliaji hatari ambao ni Sadio Mane wa Senegal, Cedric Bakambu wa Congo na Adam Ounas wa Algeria pamoja na Mahrez wenye mabao matatu.

Kati ya hao ni watatu tu wapo kwenye harakati za kupindua meza kibabe kwani bado wana mchezo mmoja mkononi wa hatua ya fainali itakayochezwa leo.

Wachezaji hao ni Mane wa Senegal, Mahrez na Ounas wa Algeria ambao wana mabao matatu na leo wanacheza mchezo wa fainali.

Wengine wenye mabao mawili ni pamoja na Belaili wa Algeria mwenye mabao mawili huku Idrisa Gueye wa Senegal ana bao moja.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic