JUMA Kaseja, mlinda mlango namba moja wa kikosi cha KMC ambaye ameitwa pia kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania kitakachocheza michuano ya Chan amesema kuwa siri ya kudumu kwenye ubora wake ni nidhamu.
Tanzania itamenyana na Kenya Julai 28 uwanja wa Taifa na inatarajia kuingia kambini Julai 21.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kaseja amesema kuwa mchezo wa mpira una kanuni zake za msingi zikifuatwa hakuna kinachoharibika.
"Wengi wanasema wanavyojiskia ila ukweli ni kwamba mpira una kanuni zake, nidhamu, juhudi na kuskiliza ndiko kumenifanya niwe hapa mpaka leo hakuna kingine," amesema Kaseja.
Makipa wengine ambao wameitwa na Kaimu Kocha, Ettiene Ndayiragije ni pamoja na Metacha Mnata wa Yanga na Aish Manula wa Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment