July 18, 2019


Ikiwa ni takribani siku kadhaa sasa zimepita tangu kuachia ngazi kwa aliyekuwa Kocha wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali 'Mensa', mchezaji huyo wa zamani wa Yanga amesema ameamua kuingia kwenye muziki.

Mensa ambaye amekuwa akijulikana kwa mbwembwe nyingi katika wadhifa wake, ameamua kuingia kwa muziki akisema kuwa unalipa kuliko soka.

"Nataka niwambie kuwa muziki una hela, nimeamua kuingia huko.

"Muziki ni kazi yangu namba mbili ukiachana na mpira, naamini nitafanya vizuri tu."

Pondamali amesema licha ya kuachana na masuala ya soka, atazidi kuipenda Yanga kwa kuendelea kuwa mwanachama kama kawaida na si kuwa amejitoa kabisa ndani ya klabu hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic