MZEE KILOMONI WALA HAJAPOA, AJA NA TAMKO LINGINE ZITO JUU YA HATI SIMBA, MAGORI ATAJWA
Mzee Hamis Kilomoni ambaye mpaka sasa amekuwa akisisitiza kuwa hajaondolewa kwenye Baraza la Wazee wa Simba, amefunguka na kusema hatishwi na kauli za viongozi wa klabu hiyo.
Kilomoni ameamua kufunguka kuwa anatarajia kutoa kauli yake ya mwisho wiki hii atakapoitisha kikao na waandishi wa habari.
Maamuzi ya kuitisha kikao hicho yametokana na tamko la Ofisa Mtendaji wa Simba, Crescentius Magori ambaye juzi alisema kuwa Kilomoni wala hana hati ya Simba hivi sasa.
Magori aliamua kuweka wazi kuwa Kilomoni amekuwa akiwadanganya watu kuwa hati ya klabu hiyo anaishikilia lakini si kweli kwa kuwa tayari mahakama imeshatoa tamko huko hatambuliki.
Kufuatia tamko la Magori, Kilomoni ameeleza kuwa atazungumza na wanahabari na akieleza Magori kuwa ni mtu wa kawaida ndani ya Simba wala hajatishika naye.
Wakupuuzwa mtu mzima hovyo.
ReplyDeleteHabari za huyo mzee mbumbu tumeshazichoka kwani imeshabaki historia na maisha yanaendelea.Magori aliita press conference na akatoa ushahidi wa nyaraka za serikali zinazoenyesha trustees halali wa Simba.Usibishane na mbumbu au vinginevyo utaonekana wewe ndio mbumbu.Huyo Mzee Kilomoni kama ana ubavu aje Simba day ndio tutajua mbivu na mbichi.
ReplyDelete