KOCHA Mkuu wa KMC, Jackson Mayanja amesema kuwa kwa sasa ameshaanza kazi kukinoa kikosi hicho kwa ajili ya michuano ya Kagame Cup inayotarajiwa kuanza mwezi Julai nchini Rwanda.
KMC
imepangwa kundi A ambalo lina timu kama TP Mazembe ya Congo, Rayon Sports ya
Rwanda na Atlabara ya Sudan Kusini na bingwa mtetezi ni Azam FC.
Mayanja
amesema atawatumia wachezaji wote waliosajiliwa na KMC bila kuwabagua kwani
anaamini wana uwezo mkubwa hali inayompa nguvu ya kuleta ushindani.
Mpaka sasa
tayari KMC imesajili majembe mapya Saba huku nyota 14 wakiongeza kandarasi
kuitumikia timu hiyo ambayo itashiriki pia michuano ya kimataifa kwenye kombe
la Shirikisho.
Majembe mapya
ni:-Salim Aiyee ambaye amesaini kandarasi ya miaka miwili akitokea Mwadui FC, Mohamed
Samata amesaini kandarasi ya miaka mitatu akitokea Mbeya City, Ismail Gambo
amesaini miaka mitatu ametokea Azam FC.
Vitalis
Mayanga amesaini kandarasi ya mwaka mmoja ametokea Ndanda FC, Kenny Ally
amesaini kandarasi ya miaka miwili ametokea Singida United na Amos Charles amesaini miaka mitatu ametokea
Mbao FC na Ramadhan Kapera amesaini kandarasi ya miaka miwili akitokea Kagera Sugar.
Walioongeza
mikataba ni James Msuva (2), Aron Lulambo, Juma Kaseja, Denis Richard, Rayman
Mgungila, Ally Ramadhan, Kelvin Kijiri, Hassan Kabunda, Charlse Ilanfia, Cliff
Buyoya, Sadala Lipangile, Rehan Kibingu, Omary Ramadhan, Abdul Hillary wote
wameongeza kandarasi ya miaka mitatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment