UONGOZI wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umesema kuwa sababu kubwa zilizofanya msimu uliopita kuwe na viporo vingi kwa timu ni kubadilishwa kwa ratiba ya michuano ya CAF.
Wilfred Kidao Katibu Mkuu wa TFF amesema kuwa :"Changamoto kubwa kwenye ratiba ya ligi ilitokana na CAF kubadilisha kalenda yake ya mashindano wakati ligi yetu ilikuwa tayari imeanza,".
Msimu mpya wa ligi unatarajiwa kuanza Agosti 17 mwaka huu kwa mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Simba vs Azam FC kabla ya mechi ya ufunguzi kupigwa Agosti 23 kati ya Simba vs JKT Tanzania uwanja wa Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment