July 20, 2019

WILLFRED Kouroma mshambuliaji wa Biashara United raia wa Ivory Coast ameingia kwenye rada za uongozi wa Kagera Sugar ambao wanaimarisha kikosi.

Inaelezwa kuwa Kagera Sugar wanahitaji huduma ya Kouruma ambaye ataziba pengo la Kassim Khamis ambaye ametimkia Azam FC.

Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa kazi kubwa kwa msimu ujao ni kuleta ushindani msimu ujao.

"Hesabu zetu ni kuona msimu ujao tunaleta ushindani hivyo usajili wetu lazima uwe makini, kuhusu huyo nyota wa Biashara bado hatujakamilisha mipango ikikamilika tutaweka wazi," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic