HATIMAYE, Farouk Shikalo mlinda mlango mpya wa kikosi cha mabingwa wa kihstoria, Yanga amewasili nchini Tanzania.
Shikalo amewasili Dar akitokea nchini Kenya ambapo alikuwa kwa mapumziko ya muda baada ya kukamilisha majukumu ya timu ya Taifa ya Kenya pamoja na klabu yake ya Bandari iliyokuwa inashiriki michuano ya Kagame.
Amepokelewa na Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten, atajiunga na timu kambini Morogoro muda wowote kuanzia sasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment