KASSIM
Khamis, mshambuliaji wa Kagera Sugar ambaye alifunga moja ya bao walipocheza na
Simba uwanja wa Kaitaba ambapo Simba ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 yupo
kwenye mazungumzo ya mwisho na Azam FC.
Habari za
ndani zimeeleza kwamba kwa sasa Azam FC tayari wamekamilisha usajili wa
wachezaji wa nje hivyo anahitajika mchezaji mmoja wa ndani ambaye ataongeza
nguvu ndani ya kikosi.
“Tayari
wachezaji wa nje kocha Ettiene Ndayiragije ameshamalizana nao hivyo kwa sasa
anamtafuta mchezaji mmoja wa ndani ambaye ataleta ushindani, yule mshambuliaji
wa Kagera Sugar, Kassim anaangaliwa kwa
ukaribu,” kilieleza chanzo.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffari Mganga amesema kuwa suala la mchezaji atakayesajiliwa ndani ya Azam FC lipo mikononi mwa kocha mwenyewe.
0 COMMENTS:
Post a Comment