July 3, 2019

KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kesho kinatarajiwa kutia timu nchini baada ya kushiriki michuano ya Afcon kwa mara ya pili.

Stars ilikuwa kundi C lililokuwa na timu kama Kenya, Senegal na Algeria na imekamilisha michuano kwa kupoteza michezo yote mitatu.

Mchezo wa ufunguzi ilipoteza mbele ya Senegal kwa kufungwa mabao 2-0 kabla ya kupambana mbele ya Kenya na kupoteza kwa kufungwa mabao 3-2 na mchezo wa mwisho ilipoteza mbele ya Algeria kwa kufungwa mabao 3-0.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo amesema kuwa ni matokeo ya maumivu kwa mashabiki hivyo kushiriki kwao ni muda wa kujifunza kutumia makosa ambayo yametokea.

"Timu inatarajiwa kuwasili Alhamisi hivyo ni wajibu wetu kujitoa na kuipokea timu yetu kwa ajili ya kuwapa moyo wachezaji wetu," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic