Mwadui FC imeshinda vita ya kuipata saini ya beki wa Mtibwa Sugar, Rojas Gabriel ambaye amesaini kandarasi ya mwaka mmoja.
Gabriel alikuwa anawindwa na timu ya Kagera Sugar , Singida United na Namungo ambapo Mwadui FC waliikomalia saini yake mpaka akakubali kumwaga wino.
Akizungumza na Saleh Jembe, Gabriel amesema kuwa anafurahi kupata changamoto mpya atapambana kutimiza majuku yake.
"Kazi yangu ni mpira na kwa sasa nitakuwa na changamoto mpya, hakuna kitakachoharibika kikubwa kupambana," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment