July 16, 2019


Nyota wa Simba, Ibrahim Ajibu amesema kuwa mashabiki wa Simba watulie watakubali mziki wake kwani amejipanga kufanya maajabu.

Ajibu ambaye msimu uliopita wa 2018-19 alikuwa kinara wa asisti ndani ya ligi akiwa nazo 17 na pia alitupia mabao sita kwa sasa ni mali ya Simba ambapo amesaini kandarasi ya
miaka miwili.

“Bado msimu haujaanza, utakuwa muda mzuri kwetu kujipanga vema kwa ajili ya msimu ujao.

“Kila kitu kwa sasa kipo freshi, natambua ushindani ni mkubwa na kila mmoja anataka kuonyesha uwezo hilo sina tatizo nalo ninaamini kila kitu kitakuwa sawa na mashabiki watapenda wenyewe,” alisema Ajibu ambaye alikataa ofa ya TP Mazembe hivi karibuni.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic