July 15, 2019


Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Mshindo Msolla, amesema kuwa lengo lao msimu ujao kunako Ligi ya Mabingwa Afrika ni kufika hatua ya makundi.

Msolla amesema malengo yao ni hayo kutokana na mashindano kuja kama bahati kwao na walikuwa hawatarajii kushiriki.

"Lengo letu kwenye klabu bingwa (CAF Champions League) ni kufika makundi ingawa nafasi ilikuja bila kutarajia.

"Kuhusu ligi kuu tunaomba waamuzi wachezeshe vizuri maana msimu uliopita walikuwa wanachezesha kwa ajili ya timu moja tu"

11 COMMENTS:

  1. Yanga Mtake msitake uwekezaji mkubwa unatakiwa....michango ya wananchi/wanachama/mashabiki pesa za viingilio kwenye mechi, kuuza jezi hakuwezi kuwafanya kuwekeza kwenye miundo mbinu (kama ujenzi wa viwanja, akademi, hostel) na kusajili na kuwahudumia wachezaji wenye uwezo Africa, kuwa na benchi la ufundi la kisasa.....lazima mtafute wawekezaji 3 au 2. Pia preseason trials na timu za chini sio idea nzuri mashindano ya CAF yanakuja lazima friendly matches mpate zile zenye viwango vya juu....mnaweza mkafanya ziara katika nchi jirani....lakini sio kucheza na Nkamba Rangers au Mawenzi Market sio kipimo kizuri

    ReplyDelete
  2. Haya basi waamuzi safari hii watachezesha kwa ajili ya timu 20 na sio 1

    ReplyDelete
  3. Kauli hizo Ni kama zile za Zahera ns kupata Yanga nafasi ya kushiriki mashindano ya klabu bingwa Afrika ni kutokana na mafanikio ya Simba katika mashindano hayo kwahivo tunasema Asante Simba na kutokana na kufanya vizuri kwa Yanga na Simba katika mashindano hayo msimu ujao milango ya heri ikazidi kufunguka. kila la heri Kwa timu zetu mbili

    ReplyDelete
  4. Unaanza kulia kabla hata hujapigwa. Hii tabia mbaya sana na ni ya mtu asiyejiamini. Mbona mnaanza kuogopa mapema mno

    ReplyDelete
  5. Mfike makundi caf au cuf.kama ni cuf sawa ila kama ni caf jamani pesa hamna bado mjipange

    ReplyDelete
  6. ameshaanza visingizio mapema profesa mzima unakuwa sawa na asiyesoma

    ReplyDelete
  7. Msingetembeza bakuli.Mpira pesa.Bila uwekezaji mtatafuta visingizio sana.Mtalaumu sana marefa ili kuwadanganya mashabiki wenu.

    ReplyDelete
  8. Si mlikuwa mnalia na migomo isiyokwisha Kwa kutolipwa wachezaji haki zao na mwisho kukimbiwa na wachezaji kilichosababisha yote hayo sio ukosefu WA pesa na jee kilichosaidia sio mzunguko WA bakuli kila Kona vipi leo unatamka kuwa pesa siyio insyochezesha hebu bakuli lisite kazi mtazame

    ReplyDelete
  9. Kikosi nakiami kitafika mbali kilabu bingwa huku kwenye ligi hakuna shaka yeyote kuhusu ubingwa

    ReplyDelete
  10. Kikosi nakiami kitafika mbali kilabu bingwa huku kwenye ligi hakuna shaka yeyote kuhusu ubingwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic