July 15, 2019



KOCHA Mkuu wa Senegal, Aliou Cisse amesema kuwa mchezo wa fainali hautakuwa mwepesi kutokana na timu zote kuwa vizuri.

Senegal imetinga hatua ya fainali kwenye michuano ya Afcon inayoendelea nchini Misri kwa ushindi wa bao 1-0 la kujifunga kupitia kwa Dylan Bronn dakika ya 100 baada ya dakika 90 kukamilika bila kufungana.

"Utakuwa mchezo mgumu hasa ukizingatia ni timu ambayo tulikuwa nayo kundi moja hivyo kila mmoja amejipanga kuibuka na ushindi tutapambana," amesema.

Djamel Belmadi kocha wa Algeria ambaye timu yake imetinga fainali baada ya kuibamiza Nigeria mabao 2-1 amesema kuwa malengo ya timu ni kupata ushindi na wanaamini watacheza na moja ya timu bora.

"Mchezo hautakuwa mwepesi ila tunawaheshimu wapinzani wetu tunafurahi kutinga hatua ya fainali kwetu ni jambo la furaha," amesema.

Timu zote zilizotinga hatua ya fainali zilikuwa kundi C ambalo lilikuwa na timu mbili za Afrika mashariki ambazo ni Kenya na Tanzania, walipokutana kwenye hatua ya makundi Algeria alimbamiza Senegal kwa bao 1-0.

3 COMMENTS:

  1. Toka mwanzo niliwaambia Senegal na Algeria ni miongoni favourity teams. Kushangaa Tz kufungwa na hizi team ni kichekesho. Halafu waandishi uchwara mnasema team imeboronga, tuna wachezaji gani wa kuhenyeshana na hawa?

    ReplyDelete
  2. Ni kocha mwenyewe ndie aliewahkikishia watanzania kuwa watarajie makubwa. Na kilichowachefua watanzania kwa Taifa stars Afcon sio kufungwa na Senegal au Algeria bali ni jinsi timu ilivokuwa inacheza mpira wa hovyo.Hawa senegali si kipindi kirefu walikuwa si chochote kwenye soka la Africa ila siku walipopata nafasi kama ya Tanzania kukipiga Afcon hawakufanya makosa ya kijinga kama yetu. Walikinukisha mbaya hadi aibu na kuzifanya timu kadhaa mbali mbali duniani hasa za barani ulaya na America kuanza kuwafuatilia wachezaji wao. Na ndio maana hii leo wachezaji wa kisenegali wametapakaa karibu klabu zote kubwa Dunuani. Kama timu ya Taifa, Taifa stars nini hasa cha kujivunia Afcon? Nnaimani kabisa kama Uganda Cranes timu ya Taifa ya Uganda kama wangelikuwa hawana uhakika wa kufuzu kwenye mechi ya mwisho na Tanzania basi taifa stars hata huko kufuzu Afcon tusingefuzu na huo ndio ukweli. Tumefuzu tumekwenda kufungwa mechi zote. Tumekwenda kucheza mpira wa hovyo. Tumeshindwa kwemda kuwa expose wachezji wetu wakiwa katika ubora kutokana na mfumo mbovu wa kocha.Kwani khassani Mwakinyo nani alikuwa anamjua? alijulikana vipi duniani? Alijulikana kwa sababu alipopata nafasi ya kupambama na bondia aliekuwa bora zaidi yake alijua kabisa ile ndio ilikuwa nafasi yake kutambulika na si wakati wa kuzembea. Taifa stars kupangwa kundi moja na Algeria na Senegal ilikuwa bahati isiokuwa na maelezo na kuna timu kadhaa zilitamani kuipata nafasi ile ya Tanzania. Kwa sababu mabosi wa Everton, Liverpool,Napoli,Barcelona,Manchester city na timu kadhaa kubwa barani ulaya na Duniani walikuwa wakifuatilia wachezaji wao kwenye Afcon na hapana shaka wakiwafuatilia wapinzani wao pia lakini je taifa stars ilionyesha kitu gani cha kuvutia? Kwa maoni yangu kwa kipindi tu kocha wa Taifa stars alijua tutakutana na Algeria na Senegal lakini je kocha alikuwa na mikakati yeyote ya kuzitumia hizi timu kwa faida? Na kama ule ulikuwa ndio mwisho wa uwezo wa Amunike katika mbinu za kufundisha mpira na tunaishia kucheza mpira wa namna ile sasa kuna faida gani ya kuendelea kocha wa aina hiyo? Time is money we can't afford to loose it.Ingekuwa faraja kuona anagalau wachezaji wetu wawili wa stars wametusua kupitia Afcon lakini tumetoka kapa sasa nini tafsiri ya mafanikio kwa Taifa stars Afcon? Ikiwa wanaigeria wanamlalamikia kocha wao aliewafikisha nusu fainali kuwa hakuwa anastahiki kuifundisha timu yao ya taifa. Sisi watanzania bado tunaendelea kumsifia na kumtetea kocha alieiongoza timu yetu ya Taifa kwa ushiriki wa aibu Afcon hapo ndipo unapojua kuwa tatizo sio wachezaji wa Taifa stars bali tatizo ni akili za baadhi ya watanzania zinazowaongoza wachezaji hao kuwa bado zimelala usingizi wa kufa.

    ReplyDelete
  3. Comment moja ndefuuuu na ndipo utaelewa sisi Watanzania tulivyo, maneno mengi sana. Tanzania bado tuna safari ya kuiendea ili kufika walipo wenzetu. Hakuna shortcut. Naungana nawe Winchislaus..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic