July 22, 2019


FEISAL Salum, Metacha Mnata,Paul Godfrey ambao ni nyota wa Yanga waliokuwa kambini Morogoro, jana wameripoti kwenye kambi ya Timu ya Taifa 'Taifa Stars' inayojiaandaa kucheza mchezo wa kufuzu michuano ya Chan dhidi ya Kenya.

Stars itamenyana na Kenya Julai 28 uwanja wa Taifa na michuano hiyo inatarajiwa kufanyika mwaka 2020 nchini Cameroon.

Kambi ya timu ya Taifa itakuwa kwenye hotel ya APC, Mbweni maalumu kwa ajili ya mchezo wa michuano ya Chan utakaochewa uwanja wa Taifa, Julai 28.

Wachezaji wengine ambao wamesharipoti kambini kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ni pamoja na Paul Ngalema wa Namungo FC, Idd Mobby wa Polisi Tanzania., Juma Kaseja wa KMC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic