July 21, 2019


JUMA Kaseja mlinda mlango wa timu ya Taifa na timu ya KMC amesema kuwa ni muda wa Taifa kuungana kupeperusha Bendera ya Taifa.

Kaseja amejumuishwa kwenye wachezaji 26 watakaopambana na timu ya Kenya Julai 28 kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Chan itakayofanyika mwaka 2020 nchini Cameroon.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kaseja amesema kuwa Taifa linapaswa liungane kwa sasa kufikia mafanikio makubwa.

"Taifa ni letu sote, kazi yetu ni kuungana na kushikamana ili kufikia mafanikio, uwezekano wa kufanya makubwa upo na nafasi yetu ipo," amesema.

Mara ya mwisho Kaseja kuitwa kikosi cha Taifa ilikuwa ni mwaka 2013, ataungana na nyota wengine ambao ni Metacha Mnata na Aish Manula kwenye nafasi ya ulinda mlango.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic