July 17, 2019


UONGOZI wa Simba umepanga kuwatoa kwa mkopo wachezaji wake Saba ambao wamekosa namba ndani ya kikosi cha kwanza.

Ofisa Mtendaji wa Simba, Cresnticentius Magori amesema kuwa tayari wamefika makubaliano mazuri na wachezaji wao hivyo kwa sasa wanakamilisha hatua za mwisho.

Wachezaji ambao wanatolewa kwa mkopo ni pamoja na  Mohamed Ibrahim (Mo), ambaye anaweza kujiunga na Namungo FC ya Lindi, Marcel Kaheza ambaye anaweza kujiunga na timu ya Singida United, Mohamed Rashid anaweza kujiunga na timu ya JKT Tanzania.

Adam Salamba anaweza kujiunga na timu moja ya nchini Afrika Kusini pamoja na Paul Bukaba na Abdul Athumani wa timu ya vijana ya U20 yeye anaweza kujiunga na Kagera Sugar.


Asante Kwasi ambaye mkataba wake unamalizika Novemba imeelezwa kuwa anaweza kujiunga na moja ya timu hapa Bongo na Lipuli pamoja na Mbao zinatajwa kuiwinda saini yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic