KALIDOU Koulibary beki mahiri wa timu ya Taifa ya Senegal leo ataukosa mchezo wa fainali kwenye michuano ya Afcon dhidi ya Algeria nchini Misri.
Hii inatokana na beki huyo kisiki kuwa na kadi mbili za njano.
Inakuwa ni mara ya kwanza kwa Senegal kumkosa nyota wao anayekipiga kwenye timu ya Napol ya Italia.
Hili ni pigo kwa Senegal kwani ni miongoni mwa mabeki tegemeo na katika michezo yote waliyocheza Senegal imefungwa bao 1 pekee na waliowafunga bao hilo ni Algeria ambao wanacheza nao leo uwanja wa Cairo.
0 COMMENTS:
Post a Comment