USAJILI YANGA WAZUA HOFU SIMBA
WAKATI kikosi cha Yanga kikiendelea kujifua huko mkoani Morogoro kwa ajili ya msimu ujao wa ligi, aliyekuwa kipa namba moja wa timu hiyo, Beno Kakolanya ametishwa na usajili uliofanywa na klabu hiyo.
Kakolanya ambaye sasa yupo Afrika Kusini na kikosi cha Simba baada ya kusajiliwa hivi karibuni, alisema kutokana na usajili huo ambao Yanga imeufanya hivi karibuni, anaamini msimu ujao timu hiyo itatisha.
Alisema kama wachezaji waliosajiliwa watakuwa na ubora ambao amekuwa akiusikia basi anaamini timu hiyo itatoa upinzani mkubwa kwa timu nyingine za ligi kuu ikiwemo timu yake ya sasa ya Simba.
“Niwapongeze tu Yanga kwa usajili walioufanya kwani kwa harakaharaka unaonekana kuwa ni mzuri jambo ambalo linaweza kutoa ushindani mkubwa kwa timu nyingine za ligi kuu ikiwemo timu yangu ya Simba.
“Ukitazama kumekuwa na mastaa wakubwa sana ambao wametajwa kusajiliwa na timu hiyo kama mchezaji lazima nijiandae vyema kukabiliana nao.
“Kwa hiyo sina mengi ya kusema zaidi ya hilo lakini niwapongeze tu kwa hilo, tukutane uwanjani,” alisema Kakolanya.
Alipoulizwa kuhusiana na nafasi ya kipa katika kikosi cha Yanga anaionaje alisema kuwa: “Makipa wote waliosajiliwa Yanga ni wazuri ila ningependa zaidi kuona Ramadhan Kabwili pamoja na Metacha Mnata ndiyo wanakuwa tegemeo katika kikosi hicho.”
Sasa usajili wa Yanga umezua hofu kwa simba au kakolanya? Ukisikia Uandishi uchwara ndio huu.
ReplyDeleteWakati mwingine waandishi warudi shuleni
ReplyDeleteHahahaha mikia bwana asa mnatoa povu la nini
ReplyDeleteWanajaribu ku balance. Lakini kila mwenye akili anaona wazi Simba ipo juu sana kwa sasa. Hata uwape moyo vipi kichapo kipo pale pale. Ili kupunguza magoli labda wapaki basi kama kawaida.
ReplyDeleteYanga haikuwa bora msimu uliopita kutokana na changamoto nyingi, naamini timu zingine zijipange kisaikolojia, tusiongelee ushabiki
DeleteYanga haikuwa bora msimu uliopita kutokana na changamoto nyingi, naamini timu zingine zijipange kisaikolojia, tusiongelee ushabiki
DeleteWasubiri kupaki basi kama kawaida yao. siku zote PROPAGANDA FC wakicheza na mnyama fomesheni yao inakuwa 9,1,0
ReplyDelete