SIMBA YAMALIZANA NA KIFAA KUTOKA TP MAZEMBE, KILIWAHI KUCHEZA KOMBE LA DUNIA
Kazi ya kusajili wakali watakaohakikisha kikosi cha Mabingwa kinazidi kuwa tishio kwa wapinzani inaendelea.
Mshambuliaji raia wa Congo DR, Deo Kanda (29) amejiunga na Mabingwa wa nchi Simba SC.
Kanda amesaini mkataba wa mwaka mmoja kukipiga Msimbazi akitokea TP Mazembe ambapo alikuwa mmoja wa wachezaji ambao waliiwezesha kushinda Ubingwa wa Afrika mwaka 2009, 2010 (aliifungia goli kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Esperance) na 2013.
Kanda pia akiwa ameshiriki Kombe la Dunia la Vilabu mwaka 2009, 2010, 2013.
Mbona hayupo Timu ya Taifa ya DRC? Tuliahidiwa kila pro atakayesaini Simba mwaka huu awe ana namba kwenye National team.
ReplyDeletekweli kaka
DeleteMchezaji kacheza kombe la Dunia kwa ngazi ya klabu halafu mtu anauliza mbona timu ya taifa hayumo? Huyu keshapita ngazi ya taifa ni wa ngazi ya Dunia
ReplyDeleteAcha kutoa utumbo wewe
DeleteNimekumbuka wakati Clatous Chama anasajiliwa Simba na kutambulishwa pale Simba day hakupokelewa kwa vishindo lkn sasa hivi ni mmoja wa wachezaji anayeimbwa kila siku pale Msimbazi.Ligi za kitaifa na kimataifa zote ni mwezi ujao August na ndio tutawahukumu.
ReplyDelete