Na Saleh Ally, Cairo
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike ameendelea kusisitiza kwamba yeye hana cha kulaumiwa.
Amunike amesema mara baada ya Stars kupoteza mchezo wake wa mwisho katika michuano Afcon.
Taifa Stars ilifungwa mechi zote tatu za michuano hiyo kwa kukubali mabao nane katika mechi tatu huku ikifunga mawili.
Baada ya mechi ya mwisho baada ya Stars kulala kwa mabao 3-0 kutoka kwa Algeria, Amunike amuse a hana cha kulaumiwa.
“Nilaumiwe kwa lipi? Mimi ni kocha na timu uliiona. Hapo ndipo tulipofikia na nilichofanya sikuwa na zaidi ya kuongeza,” alisema.
Hata alipoulizwa kwamba ana maanisha hakuwa na uwezo wa kuongeza chochote cha kuiokoa au ana maanisha hakuwa na uwezo zaidi ya hapo, akajibu.
“Mimi nimemaliza, indigo tulipofikia, ahsante.”
MECHI ILIZOPOTEZA TAIFA STARS:
Vs Senegal 2-0
Vs Kenya 3-2
Vs Algeria 3-0
Sasa kaonesha dharau gani huo ndio ukweli wenyewe tatizo tunapenda maneno ya kuriwazana tuu. Timu imeweka kambi wiki moja Dar ikamalizia Misri wenzenu wameweka kambi za maana kujiandaa eti mnategemea mpate ushindi kirahisi hovyo kabisa. Tuwekeze siriasi kwenye mpira tuache porojo.
ReplyDeleteFact
DeleteHIVI ULITAKA KOCHA ASEME NINI ZAIDI? NI JUU YA MWAJIRI WAKE SASA KUAMUA KAMA ANAONA UWEZO WA KOCHA UMEFIKIA KIKOMO NA KAMA ANATAKA MAFANIKIO ZAIDI AU YA HAPO TULIPOFIKA YAMETOSHA.
ReplyDeleteTatizo waandishi wetu hata lugha shida huenda hakumuelewa kabisa kocha na kibaya zaidi wamezoea interview simple kutoka kwa kina Julio na Masau Bwire. Jiongezeni wakubwa.
ReplyDeleteHapo kilichobaki ilikuwa aingie mwenyewe kocha
Kocha bomu zamani sana ila TFF ni bomu zaidi.
ReplyDelete