July 14, 2019




Tambwe amepaza sauti kutoka Burundi hadi Tanzania akimtaka Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amrudishie kitambaa cha unahodha beki Kelvin Yondani.


Yondani alipewa kitambaa cha unahodha kwenye mechi za maandalizi za msimu uliopita baada ya beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kustaafu lakini baadaye Yondani alivuliwa kwa madai ya utovu wa nidhamu.


Tambwe amesema; “Tusubiri tuone kama Zahera atakubali ushauri kuhusu hili la kumrudishia Yondani kitambaa japokuwa nafahamu ana misimamo yake na kila mtu anaijua, hakuna mchezaji anayestahili kuwa nahodha zaidi ya Yondani.”


“Kwanza kabisa ni mchezaji mzoefu lakini pia kwa sasa ndiye mchezaji mkongwe katika kikosi hicho kuliko wengine wote na ana heshimika na kila mchezaji kutokana na uwezo wake uwanjani.”

2 COMMENTS:

  1. Tambwe ana mapenzi makubwa na timu yake na ikiwa kapoteza kiwango arejeshwe awe angalau mshauri

    ReplyDelete
  2. Tambwe anashauri vyema kama kocha atakuwa muungwana ataupokea ushauri.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic