JOSE Mourinho kwa sasa anafikiria kurejea kwenye benchi la ufundi akiwa ni meneja endapo atapata timu sahihi.
Mourinho mwenye miaka 56 amekuwa bila timu kwa muda mrefu baada ya kupigwa chini ndani ya kikosi cha Manchester United, Desemba mwaka jana.
Amekuwa akihusishwa kujiunga na timu ya Benfica msimu ujao, Lyon na Newcastle United wametajwa kumhitaji bosi huyo ambaye ameinoa pia Chelsea na Real Madrid.
"Mpango wangu kurejea kazini upo na nina hasira ya kazi ila kwa sasa ninasubiri timu sahihi ambayo nitaifundisha nikiwa na mipango sahihi.
"Wakati sahihi ukifika nitafanya mambo ambayo nimewahi kuyafanya ninapenda kazi na ninapenda pia michezo mingine mbali na mpira naona kwa sasa ni muda wangu wa kufurahia," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment