OLE Gunnar Solskjaer, Meneja wa Manchester United amesema kuwa klabu hiyo haina mpango wa kumuuza staa wa timu hiyo Paul Pogba.
Pogba hivi karibuni alifunguka kwamba hana mpango wa kubaki ndani ya kikosi hicho anahitaji kupata changamoto mpya.
"Manchester United ni klabu kubwa, kwa hiyo hailazimiki kuuza mastaa wake, suala la kuamua kama nitabaki na mchezaji gani ama nani nipo tayari kumuuza siwezi kulizungumzia.
Pogba amebakiza miaka miwili ndani ya klabu hiyo yupo na timu nchini Austaralia kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.
0 COMMENTS:
Post a Comment