July 16, 2019

 GADIEL Michael beki wa Simba na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' amesema kuwa ishu ya namba ndani ya timu yake mpya anamuachia Kocha Mkuu, Patrick Aussems ambaye ni raia wa Ubelgij.

Gadiel amesema kuwa haoni haja ya kuanza kufikiria namna gani atacheza ila kikubwa anajipanga kufanya vema kwa ajili ya manufaa ya timu.

"Sina mpango wa kugombania namba, hilo suala lipo chini ya kocha yeye ndiye ataamua nani aanze na nani asubiri hivyo sina tatizo na ushindani utakaokuwepo.

"Ushindani upo kwani kila mchezaji ana uwezo wake, lakini mwisho wa siku mwalimu ndiye anayepanga kikosi," amesema.

Gadiel ni beki wa kushoto anacheza namba moja na nahodha msaidizi Mohamed Hussein 'Tshabalala,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic