INTER Milan sasa wanatakiwa kulipa dau la pauni milioni 90 ili kumpata mshambuliaji wa Manchester United, Romelu Lukaku.
Raia huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 26 anahusishwa kujiunga Milan na kukikacha kikosi cha United kilicho chini ya meneja ole gunnar solskjær ambaye amesema kuwa hawezi kuweka wazi kama anahitaji kubaki naye ama la.
"Kile ambacho huwa naongea na wachezaji wangu tukiwa kwenye vyumba itabaki kuwa siri yangu na sitasema kamwe kama nahitaji Lukaku aondoke ama la," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment