Na Dominick Salamba
Miaka ile ya 1990, enzi za ujana wetu kipindi cha ujana wetu wakati muziki kutoka Kongo ukitamalaki katika nchi yetu zama zile muziki huu ulikuwa unaitwa disco toto ambapo zilikuwa zikifika siku za sikukuu tulikuwa tuna ulamba nguo mpya,viatu vipya huku wengine wanatinga miwani na wengine kapelo halafu wote tunaelekea kwenye kumbi za disco ambazo zilikuwa chache sana na kutufanya tujazane na kugombana milangoni ili tu tuwahi kuingia ndani.
Kitu cha ajabu ambacho kilikuwa kinanifikirisha ingawa nilikuwa katika umri wa utoto ni pale ambapo tuliingia ukumbini na kukuta mazingira ya ukumbi yalivyo, ukumbi haukuwa na sakafu ni mwendo wa vumbi, hakuna vyoo na kama vipo ni vichafu,mazingira ya kukaa hakuna yani ni vurugu tu unaingia msafi ila unapotoka ni afadhali hata mtu aliyetoka shamba na kujikuta zile nguo ulizozisubiri kwa mda mrefu kuchafuka vibaya na kupoteza unadhifu wake.
Ila kwakuwa hatukuwa na njia mbadala na tulipenda muziki turirudi tena na tena ingawa ubora na thamani ya kile tulichokifuata hakukipata kwa kiwango tulicho tamani kukipata.
Achana na zama za Dominick Salamba turudi kwenye mada yetu ambapo tulio wengi ni wadau na wapenzi wa mchezo wa soka mchezo ambao pengine sisi mashabiki na watazamaji tumekuwa tukipata raha zaidi kuliko hata wanaocheza mchezo ambao umegusa hisia na akili za mashabiki wengi mchezo ambao kuna watu wamepoteza maisha kutokana na ushabiki na mapenzi yaliyopitiliza.
Hii yote ni burudani iletwayo na huu mchezo,tofauti yake huu mchezo uchezwa uwanjani sio chumbani au sebuleni au ukumbini uwanja ambao unakua na sehemu kuu mbili kwa maana sehemu ya kuchezea mchezo wenyewe na sehemu ya watazamaji ambao hawa ndio wenye burudani.
Tukianzia kwenye sehemu ya kuchezea hapa ndipo penye utamu,kwa maana ya kuona uwezo wa timu namna inavyocheza ubora wa mwalimu kwa maana ya mifumo na uwezo wa kusoma timu pinzani lakini pia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja ubunifu,unyumbulifu,na mengine mengi ili tu timu ipate matokeo na kuendeleza furaha kwa mashabiki wao,lakini haiishii hapo tu ni sehemu inayotakiwa kuwa bora zaidi ili kutoa fursa hata kwa waamuzi kuweza kuumudu uwanja.
Kwani wanatakiwa kuona mipaka ya uwanja hili litawezekana endapo kama uwanja utakua upo katika msawazo ulio sawa,na pia kuwepo kwa vitu kama wavu katika magori,alama zinazo onekana vibendera na uzio ambao utatenga eneo la mashabiki pamoja na eneo la kuchezea uku wale wachezaji wa akiba pamoja na mabenchi ya ufundi yakipata sehemu safi na zenye ubora wakati wakiendelea kufanya kazi ya kutoa maelekezo wakati mchezo unaendelea kwani wanakuwa na kazi ya kutoa maelekezo kwa walio ndani na wale walio benchi uku wakiangalia mapungufu ya timu zao na ubora pia na kutumia mapungufu kama sehemu ya wao kutafutia ushindi.
Upande wa pili ni upande wa jukwaa ambao mashabiki ndio ukaa na kutazama mechi haijalishi kama wengine watasimama mda wote kutokana na mizuka yao wengine wakakaa uku wakitazama kwa utulivu mchezo unavyokwenda yote kwa yote hawa wote wanahitaji mazingira yaliyo safi na salama ili waweze kupata burudani kwa kadri ya wanavyopaswa kuipata.
Eneo hili linatakiwa kuwa na usafi wa jumla,miundombinu rafiki kama uwepo wa vyoo safi na vya kutosha,sehemu safi za kukaa,upatikanaji wa huduma kama chakula,vinywaji,vitafunwa na vingine vingi uku ulinzi wa watu na mali zao ukiwa ni wa kiwango cha juu,lakini pia namna ya kuingia uwanjani na kutoka kusiwe na ugumu wowote ikiwa sambamba na upatikanaji wa tiketi kwa urahisi ili watu wa aina zote waweze kushawishika kuja viwanjani.
Hivyo kwakuwa mchezo huu una mamlaka ambazo zinasimamia ni jukumu lao sasa kuona namna ya kuboresha miundombinu kwani watu wanaenda viwanjani kupata burudani na wakati huu ambao tunawataka wapenzi wa soka waende uwanjani isiishie kuwaomba tu bali kutengeneza mazingira kwa vitendo ili watu washawishike kutokana na miundombinu rafiki.
Kuna wakati vilabu vinajiandaa vizuri vinatumia gharama kubwa kwenye maandalizi na kusajili wachezaji ili wapate matokeo ila mazingira ya viwanja vyetu yanatuangusha na kuna wakati tumeshuhudia viwanja vikiwa havina watu kwakuwa mazingira sio rafiki ikiwa na namna ya upatikani wa tiketi unakua na urasimu usio na sababu kwa tutambue kuwa moja ya vyanzo vya mapato katika vilabu vyetu ni viingilio vya uwanjani.
Lakini pia mapato hayo huwa hayaishii tu kugawanywa kwa vilabu husika bali hata vyama vya mikoa vinapata asilimia fulani hivyo kwa mkusanyo huo ni vema wakaangalia namna ya kuboresha hali ya viwanja.Mara ngapi tumeshuhudia timu zikigoma kuingia vyumbani kwa madai ya vyumba kukosa ubora jambo ambalo sio afya kwa maendeleo ya soka.
Pia uwanja ni sehemu ya kufanya matangazo ya biashara na kuwa moja ya vyanzo vya mapato pia hivyo vyama vyama vya mikoa na shirikisho kuna haja ya kuona namna ya kutafuta njia ya kufanya ukarabati wa viwanja vyetu ili tupate ligi zenye ushindani lakini pia itupe uwezo wa kupata mashabiki wengi wa jinsia zote kutokana na ubora wa viwanja vyetu na kuwa ni moja ya vyanzo vya mapato.
Kwani kuna wanawake wengi wanapenda mchezo wa soka ila wanashindwa kwenda viwanjani kutokana na hofu ys usalama wao na mazingira yasiyo vutia katika viwanja vyetu.
Nategemea kamati ya kukagua ubora wa viwanja vyetu vitakavyotumika msimu ujao itafanya kazi mapema na kutoa maelekezo kulingana na vigezo vinavyohitajika na si kutumia urafiki ili kuruhusu viwanja ambavyo havina ubora na kuvifungia kwani kwa kufanya hivyo inaweza kuleta umakini na kuchukua hatua za makusudi katika kufanya marekebisho.
Naona muda unasogea na ni mida ya lunch inakaribia cha mchana kipatikane.
Salamba ni mchambuzi wa Soka anapatikana kwa namba +255713942770
0 COMMENTS:
Post a Comment