July 2, 2019







NA SALEH ALLY
MIAKA 39 michuano ya Kombe la Mataifa Afrika maarufu kama Afcon kwetu ilikuwa ni hadithi. 
Safari hii timu yetu ipo hapa jijini Cairo nchini Misri na leo itashuka kucheza mechi yake ya mwisho ya hatua ya makundi.


Suala la kusonga mbele katika hatua ya mtoano linabaki kuwa majaaliwa. Lakini uhalisia ni hivi, timu inashiriki michuano hiyo.


Kwa miaka 39, Tanzania imekuwa ikicheza dhidi ya timu mbalimbali katika hatua ya kufuzu kucheza michuano hiyo au Kombe la Dunia bila ya mafanikio.


Safari hii imecheza na Senegal kutoka Afrika Magharibi katika Afcon, hali kadhalika majirani Kenya na sasa leo Algeria.


Hii ni hatua kubwa sana ambayo kwa mafunzo na kilichoonekana katika Afcon, basi kuna kila sababu ya kuanza kujifunza na kuyafanyia kazi muhimu.
Stars ilitua katika michuano hii ikiamini iko vizuri lakini uhalisia umeonekana kwa kuwa kiwango cha timu yetu kimeonekana si kiwango bora na hakuna anayeweza kupinga.


Swali la kujiuliza, wenye viwango bora huwa wanafanya nini? Baada ya hapo unaanza kufanya kile kilicho sahihi hata kama itakuwa ni kwa miaka.


Haya yatakwenda kwa mipango ya muda mfupi na muda mrefu kuhakikisha tunafikia katika kile ambacho kinahitajika ili kufikia ubora sahihi unaoweza kuifanya Tanzania kuwa na timu itakayoshindana katika michuano hii.



Wakati tunawaza hayo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), linaweza kukubaliana na uamuzi wa kumuachia Kocha Emmanuel Amunike aende zake, lakini kwa heshima.
Nasema kwa heshima kwa kuwa anaingia katika historia ya makocha waliofanya makubwa kwa kuifikisha Tanzania katika michuano ya Afcon mara ya pili ikiwa imekaa nje baada ya miaka 39.


Kumbuka mara ya mwisho kushiriki mwaka 1980 ilikuwa nchini Nigeria na baada ya miaka 39, Mnigeria ndiye ametuvusha huko.


Wako wanapinga, wanasema si yeye. Kulikubali hilo maana yake kulikuwa na njia haramu zilizotupeleka na si kocha. Kama yupo anaweza kulithibitisha hili, basi ajitokeze na kusimama hadharani, aseme.


Mimi Amunike aende zake kwa kuwa ukiangalia tukubali sote, timu yetu haina uwezo mkubwa. Amunike kama kocha hilo ni jukumu lake.


Alitakiwa kuwainua wachezaji na kuwajengea hali ya kujiamini. Kuwa mzuri katika kuinua ari ya mechi na nguvu ya kwenda kushindana.


Hii ni kwa kuwa hali ya kujiamini ya wachezaji katika kikosi chetu haiko juu sana na inatokana na wachezaji wengi kucheza katika ligi ya nyumbani ambayo bado si kubwa au yenye nguvu sana barani Afrika.


Hata wale wanaocheza barani Ulaya au nje ya Tanzania, bado hawajaweza kufikia kucheza katika ligi kubwa zaidi ambazo zingewafanya kujenga hali ya kujiamini zaidi na wangempunguzia kazi yeye Amunike.


Mchungaji anawasoma kondoo wake na anajua njia sahihi ya kuwaongoza kupita hata kama watakuwa ni dhaifu. Hili lilimshinda Amunike.


Nimebahatika kuzungumza naye mara kadhaa, kosa kubwa nimeona analolifanya, ni kuizungumzia sana Barcelona aliyocheza na umuhimu wake kwa taifa la Nigeria.
Amejisahau yeye ni kocha, anapaswa kujishusha. 

Amejisahau yeye ni baba, anapaswa kuwa chini ili kuinuka na wanaye pamoja.


Nguvu nyingi kuonyesha hababaiki, hajali sana na yeye ni mkubwa sana. Hili ni tatizo linalomfanya kutokuwa kocha aliyeiweza meli aliyokuwa anaiongoza.


Kitu kingine, tunaweza kuwa tunamlaumu sana Amunike, huenda naye unapozungumzia ukocha, hapishani sana na wachezaji wetu kwa maana ya kiwango cha michuano ya Afcon.


Kama mchezaji kweli alikuwa bora sana lakini kama kocha naye ni mchanga. Inawezekana alijitahidi kadiri ya uwezo wake, lakini mambo yakawa ya “mustach”.


Kila jambo, lina hatua. Alipotufikisha yeye, tumpe heshima yake, tutafute mwingine anayetutoa hapa kusonga mbele na lazima awe wa viwango vya Afcon ili kutengeneza kitu tofauti kulingana na tuendako.


8 COMMENTS:

  1. Na mngepita katika hatua hii ya awali ingekuwaje? Simlaumu kocha ila nawashangaa zaidi watanzania kwa kutothamin hatua waliofikia baada ya miaka mingi. Hatuna professional wa kutosha halafu tunahitaji kwenda mbele zaid licha ya kutoshiriki katika michuano hii kwa kipindi kirefu, Salehe unadhani mpira ni sawa na kwenda kwa mzungu? Mpira ni sayansi inahitaji muda wa kutosha kuwa gulu nayo,,ila kama utataka tuwe wazee wa miujiza from no where na mpira wa midomon bila ya kuufanyia investment (in term of financially and time), broo tutasubiri tena another 39+ years kushiriki tena. Subra ndio kila kitu, hata hao wenye mpira wao they didnt fry broo...learn broo..mimi nasikitika kuangushwa na watu niliowaamin wanajua mpira kama wewe brother..sorry for this attacking

    ReplyDelete
  2. Amunike aondoke ikiwa kwa heshima au matusi.Matusi kwa kocha ni kitu cha kwaida.kocha anaweza kuipa ubingwa timu lakini msimu unaofuata akifanya vibaya akakutana na mitusi vile vile. Kipi kikubwa alichokifanya Amunike kwa taifa stars zaidi ya kutuvua nguo hadharani watanzania. Hali ilivyokuwa na hata Julio angeliipeleka stars Afcon tena sio kwa kusuasua kama ilivyokuwa kwa Amunike.
    Na kama Amunike angekuwa Muungwana basi angeomba radhi kwanza watanzania. Na amuombe raisi wetu wa nchi. Muheshimiwa raisi alimuamini sana na mpaka dakika ya mwisho amekuwa pamoja na taifa stars licha ya kuwa timu hiyo kiukweli ni ya kawaida mno kiufundi uwanjani.Magufuli ni mtu mwenye kujali ubora tena ikiwezana upatikane kwa kazi ya kipindi kifupi lakini kwa taifa stars hii ya Amunike kama kutakuwa hakuna mabadiliko kwenye benchi la ufundi basi inaweza kuchukua miaka kadhaa tena kabla ya Tanzania kurudi tena Afcon. Hata Morocco msaidizi wa Amunike na wasaidizi wake wakati umefika kuondolewa Taifa stars apishe wengine kwani hana msaada wowote wa maana kwa timu hiyo.Kunatimakikana kupitishwa ufagio kwenye benchi la ufundi la taifa stars. Kusafishwe kabisa na kuanza kuwa na muelekeo mpya wa kutafuta makocha wenye uwezo zaidi na watakaowajikibika kimkataba. Haya mambo ya kuwachekea watu wanaposhindwa kutimiza majukumu yao ya kazi ndio sababu inayotuchelewaesha na kuwa wa nyuma kwa miaka yote hii. Kwenye elimu ya kazi na majukumu yake head man au boss ama kiongizi wa kazi ndie mwenye kubeba msalaba wa lawama na wakati mwengine hata kuwajibika kwa mapungufu ya wale anaowaongoza. Sasa sijui Amumike kiburi anakipata wapi cha kutojali na kutokuwa na huzuni kwa ufanisi wa hovyo wa timu anayoifunda.

    ReplyDelete
  3. Sikubaliani na wewe Saleh Jembe. Kwa nchi yetu ya Tanzania hata aje Guardiola hatuwezi kupata mafanikio hayo ya haraka unayoyataka wewe. Naamini tungeendelea kubaki naye ingekuwa uamuzi mzuri zaidi. Tutamaliza makocha lakini kama nchi na vilabu havitawekeza katika michezo na kufanya jitihada za makusudi za kupeleka wachezaji wetu nje tena wakiwa wadogo, tutabaki hapahapa na kazi yetu ya kubadili makocha. Wenzetu Madagascar na Mauritania wachezaji wao wengi wako France ndiyo maana wanaendelea vizuri in football.

    ReplyDelete
  4. Nimeichambua makala ya Saleh na kubaini sababu 3 zinazopelekea Saleh apendekeze kutimuliwa kwa Kocha Amunike;
    1. Kwamba ni mjeuri, kila anapohojiwa na Saleh haoneshi unyenyekevu
    2. Kwamba Kocha Amunike ana uwezo mdogo kulinganisha na mashindano ya Afcon
    3. Kwamba Taifa Stars ilifungwa kwa kuwa uwezo wa Kocha kupandisha morali ya wachezaji na kuwajenga kisaikolojia ni mdogo na hivyo kupelekea vipigo.
    Kama hivi ndivyo basi tuna kazi kubwa zaidi.
    Saleh siku utakayokwenda kumhoji Mourinho utampiga.
    Professionals wengi hawajibu swali wanajibu substance au maudhui ya swali.
    Hili la 2, hivi uwezo wa Amunike ulipungua ndani ya ndege Dar -Cairo?
    Naomba kesho utuletee wasifu wa makocha wote walioifunsha Stars tangu 1980, Dr Samsarov (aka Sambusa mbovu)hadi Syllersaid Mziray, Maximo hadi Amunike. Wasifu ulikuweje dhidi ya mafanikio yao.
    Katika historia ya Kombe la Dunia Brazil ilifanya vibaya sana ikiwa chini ya Tele Santana.
    Tunahitaji tafakuri kwa mapana zaidi kuliko jazba.
    Kwamba kocha hajishushi sijui ulitaka nini? Wachezaji woote mliotaka wacheze kawapanga; Nyoni, Tshabalala, Adi Husuf sijui tunataka nini au atununulie kahawa?
    Nina hofu unaposema Afcon unalenga kitu kingine

    ReplyDelete
  5. Amunike sio kocha bali watanzania ni watu wa kubabaika na majina zaidi. Ukienda kupekua kwenye Soccer Coaches world ranks au coaches world infos Amunike huwezi kumuona kabisa sasa watanzania ni wajinga kiasi gani? Na wanosema hata aletwe kocha gani Tanzania hatuwezi kunyanyuka kisoka. Nataka atokee mwanamme aseme na athibitishe kwamba kunako kipindi cha miaka arubaini 40 kama timu ya taifa ya Tanzania yaani taifa stars iliwahi kufundishwa na kocha angalau alikuwa rekodi ya kuipeleka timu yeyote ile kunako fainali ZA Afcon? Makocha wote waloajiriwa ni wa kawaida tu.Mgonjwa sugu unakwenda kumkabidhi Daktari wa kaida unatarajia nini?

    ReplyDelete
  6. Watanzania tunatakiwa kuacha kulaumu wakati tunsahau hata ya jana, nadhani tukubabali tulikofika tumejitahidi, tunatakiwa kulaumu tukishiriki zaidi ya mara tatu, kocha siwezi kumlaumu wakulaumiwa ni TFF ambao hawatuletei kocha wa kiwango cha michuano kama hiyo.Mpira ni gharama hivyo tupate kocha ambaye hitajiki kusema eti alikuwa kwenye benchi la Brazil,hapana.aletwe kocha ambaye kila mpenda soka anamjua na amewahi kubeba au kufika fainali ya mashindano kama hayo.Leta kocha anayefundisha Moroco hapo tutalaumu tukishindwa.Aidha kwa maumbo ya wachezaji wetu nashauri kocha wa kufundisha kumiliki mpira maana kwenye nguvu tunafeli.

    ReplyDelete
  7. Tusonge mbele kwa jambo gani la maana!? Miaka 39 Amunike tulikuwa naye!? Mbona hatukwenda kokote!? Tuache kujisifia ujinga, soccer letu liko chini mno, badala ya kukaa na kusifia ujinga wa yanga na simba na tff yetu ya kutengeneza matokeo, hebu tuboreshe ligi yetu kwanza. Salehe bado soccer hulijui au unaongozwa ni mihemuko

    ReplyDelete
  8. wanaombeza salehe wote nazan wana ,uhemko au awana jicho la kuona zaidi kweli kocha ametuwezesha kufuzu lakin ebu tuangalie kwa njia gan na style hipi tuanze kwanza kwann atujafuzu kwa miaka 39 na tumefuzu sasaiv je kweli tumefuzu kwa ubora wa kocha tuseme miaka 38 yote iliyopita atukua na kocha mwenye ubora wa mfano wa omunike tukubali tukatae kua amunike ni kocha wa kiwango cha kawaida kabisa tena ata maximo amemzid kwa ukiangalia namna ya timu aliyokua nayo maximo na hii aliekua nayo amunike amekuja kipind watanzania wachezaj na mashabiki tuna matamanio makubwa ya kushirik afcon amekuja kipind ambacho wachezaj wetu wana tamaa ya kutoka nje yan kifupi ni kizazi cha dhahabu amunike pamoja na kuwakua wachezaj wazur lakin alishindwa kuiunganisha timu kuipa timu morali kama ile ya maximo na iyo ndio kaz kuu ya kocha wa timu ya taifa kocha wetu ajui mchezo mkubwa wala mdogo anapak basi mbka na lesotho tena kwenye mechi ya kutafuta ushind ajui kubadilisha mpango baada ya ule A kufel, ni kweli kocha mzur ila sijaona cha tofaut kwake BYEEEE AMUNIKE mungu alikupa bahati ya kuandika historia nasi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic