WINGA MPYA YANGA AAHIDI KUIPOKA SIMBA KOMBE LA LIGI KUU
Winga mpya matata wa Yanga Mnyarwanda, Patrick ‘Papy’ Sibomana amefurahia mapokezi aliyoyapata Jangwani na kuahidi kuifanyia makubwa timu hiyo ikiwemo kuipa mataji ya ubingwa.
Kauli hiyo aliitoa Mnyarwanda hivi karibuni akiwa kambini mkoani Morogoro wakijiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika, mwaka huu.
Sibomana ni kati ya wachezaji 13 wapya waliosajiliwa na Yanga kwa kwa mujibu wa mapendekezo ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera.
Sibomana alisema kuwa, anafurahia kujiunga na klabu kubwa Afrika huku akiongeza kuwa atahakikisha anatengeneza nafasi na kufunga mabao ili waweze kutwaa ubingwa wa ligi kuu unaoshikiliwa na Simba.
“Najivunia kuwepo kwenye klabu kubwa na bora Afrika, nikiwa hapa nitafungua ukurasa wangu mpya wa maisha na sitasubiria nitahakikisha ninatimiza malengo yangu.
“Kwa kuanza nitaanza na ubingwa wa ligi ambao ndiyo muhimu kwangu kwa kutumia nafasi yangu nitahakikisha ninatimiza majukumu yangu ya uwanjani ambayo ni kufunga na kutengeneza nafasi za kufunga mabao.
“Hiyo itakuwa zawadi tosha kwa mashabiki wa Yanga walionipokea na kunionyesha ukarimu mara baada ya mimi kusaini mkataba wa miaka miwili,” alisema Sibomana.
Wataelewa tu. Karibu ufanye mavituzi yako kwa wananchi
ReplyDelete