July 31, 2019

IKIWA leo dirisha la usajili linafungwa majira ya saa 5:59 usiku taarifa ya awali iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inaonyesha kuwa kuna timu bado hazijakamilisha usajili wa wachezaji

Taarifa yao ipo namna hii:-

Kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara (TPL) zote zimekamilisha tayari usajili.

 Kwa timu ambazo zinashiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL) :- Timu ya Raha haijaanza hata usajili wa mchezaji mmoja na Mufindi yenyewe imesajili mchezaji mmoja.

Kwa tmu zinazoshiriki Ligi Daraja la Pili:- Pan African, Kitoyasa, Usalama, Bulyanhulu, Dar City, Mkwamba Rangers, Forest, Rufiji/Kiluvya United, hazijaanza usajili hata mchezaji mmoja.

Toto African imesajili wachezaji wawili tu na Villa Squad imesajili wachezaji sita pekee.

2 COMMENTS:

  1. Eti ile ishu ya udhamini vipi?au mambo ya blah blah blah itaendelea na mwaka huu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic