July 17, 2019


UONGOZI  wa yanga umefunguka kuwa tayari umekamilisha suala la vibali vya kazi na makazi kwa wachezaji wao wote wapya ambao wamesajiliwa msimu huu.

Nyota wa kimataifa waliosajiliwa na Yanga kipindi hiki ni Patrick Sibomana, Juma Balinya, Maybin Kalengo, Farouk Shikalo, Issa Bigirimana, Lamine Moro, Sadney Urikhob na Mustapha Selemani.

Wachezaji hao baadhi wameshaanza majukumu yao kwa kuwa kambini mkoani Morogoro kwa maandalizi ya msimu ujao wa 2019/20 ambapo Urikhob aliwasili jana, huku Shikalo akiwa bado hajawasili nchini. Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, alisema kuwa nyota wao wote wapya wa kigeni wamekamilisha taratibu zote za vibali.

“Mpaka sasa wachezaji wetu wote wapya tumekamilisha vibali vyao vya kufanya kazi pamoja na makazi, hivyo hatuna tatizo lolote kwa upande huo.

 “Sababu ni jambo jema kufanya utaratibu mzuri mapema ili kuepusha migongano ya hapa na pale kama ambavyo ilizua utata kule uwanja wa ndege kwa Sadney na akashindwa kutua nchini siku ya Jumatatu, alipata usumbufu kutokana na utaratibu wao huko kwao, alionekana kama vibali havijakaa sawa lakini alikuwa navyo vyote pamoja na mkataba wake,” alisema Mwakalebela.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic