July 17, 2019

ETTIENE Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Azam FC, amesema kuwa siri kubwa ya timu hiyo kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kagame ni ukubwa wa timu kwenye michuano hiyo.

Azam FC ilishinda kwa mabao 2-1 mchezo wa hatua ya robo fainali na mabao ya Azam FC yalipachikwa na Iddy Naldo pamoja na Obrey Chirwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ndayiragije amesema kuwa aliwaambia wachezaji wajiamini na wanaweza kufanya makubwa mbele ya TP Mazembe.

"Niliwaambia wachezaji wasiwe na mashaka, uwezo mkubwa wanao na sisi ni timu kubwa kutokana na kuwa mabingwa watetezi wa kombe, hivyo hicho kimetubeba," amesema Ndayiragije.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amewashukuru watanzania kwa sapoti zao na dua kwa wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano hiyo baada ya KMC kuondolewa.

2 COMMENTS:

  1. Well done Azam.Jitahidini pia namlete ushindani katika ligi ya Bongo

    ReplyDelete
  2. ingekuwa simba ndio kamtoa mazembe hapo nadhani tusingekula wala knywa. lkn azam anawashukuru watanzania. na hakuna magazeti kupamba kwa lolote.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic